Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Mvutano katika Bahari Nyekundu na Mlango wa Hormuz unaendelea kuongezeka baada ya Jeshi la Yemen kutangaza operesheni mpya dhidi ya meli za mafuta za Saudi Arabia, huku Iran ikisisitiza kuwa vitisho vya Marekani haviwezi kuilazimisha kubadili msimamo wake kuhusu Mlango wa Hormuz.
Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limelenga kwa makombora ya balistiki meli ya mafuta ya Saudi "Wafaa" kaskazini mwa Bahari Nyekundu karibu na eneo la Yanbu, likidai kuwa shambulio hilo lilifanikiwa kwa usahihi. Kwa mujibu wa jeshi hilo, idadi ya meli za mafuta za Saudi zilizolengwa tangu kuanza kwa marufuku ya usafiri wa baharini imefikia nane, huku meli 29 zikidaiwa kuzuiwa au kulazimishwa kurejea katika Bahari Nyekundu na Bahari ya Arabia.
Jeshi la Yemen pia limesema Saudi Arabia imeanza kubadili njia za meli zake za mafuta kuelekea kaskazini mwa Bahari Nyekundu, likiongeza kuwa operesheni zake zitaendelea na kuongezeka hadi njia zote zitakapofungwa kwa meli za mafuta za Saudi.
Kwa upande mwingine, mwandishi wa Al Mayadeen mjini Tehran ameripoti kuwa Iran inaamini vitisho vya Marekani havitafungua Mlango wa Hormuz kwa nguvu. Aidha, ameeleza kuwa kuna hali ya matumaini nchini Iran kuhusu uwezekano wa kufikiwa makubaliano kati ya Iran na Oman kuhusu usimamizi wa mlango huo muhimu wa kimataifa, ikiwa hakutakuwa na uingiliaji wa Marekani.
Wakati huohuo, Shirika la Habari la Novosti limemnukuu afisa mwandamizi wa Pakistan akisema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anatarajiwa kuwasili Pakistan siku ya Ijumaa, ambapo atapokelewa na Waziri Mkuu wa Pakistan pamoja na viongozi wengine waandamizi kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala ya kikanda.
Nalo Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Sana'a imesema kuwa hatua zozote za Saudi Arabia za kuongeza mvutano zitakabiliwa na hatua kali zaidi, huku ikisisitiza kuwa njia ya amani ipo wazi na ndiyo suluhisho salama kwa pande zote.
Maoni yako